BUNDA yapokea viuadudu ekapack chupa 42 elfu na mabomba ya kupulizia 500 kwa ajili ya wakulima wa zao la pamba
1 January 2023, 5:51 pm
Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bunda imepokea viua dudu ekapak 42 elfu na mabomba miatano kwa ajiri ya wakulima wa zao la pamba
Akizunngumza katika mapokezi hayo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya Afisa Tarafa ya Serengeti Revocatus Mkangara amesema ni wajibu wa AMCOS akusimamia ugawaji wa pembejeo hizo kwa wakulima na kuepukana na udanganyifu
Amesema katika viua dudu hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Bunda itapata ekapak 25 elfu na mabomba mia tatu huku Halamshauri ya Mji ikipata ekapak 17 elfu na mabomba 200
Kwa upande wake mkaguzi wa zao la pamba wilaya ya Bunda Hemed Kabea amesema huu ni mwedelezo wa yale yanayofanywa na serikali kupitia bodi ya pamba huku akitoa tahadhari ya usimamizi bora wa pembejeo hizo na kuwa watafuatilia fomu zote namba tano zinazohusu ugawaji wa viuadudu katika AMCOS