Mazingira FM

Sagini awaonya madereva wazembe kuelekea mwisho wa mwaka

16 December 2022, 7:52 am

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amewataka maderava wa magari ya abiria na binafsi kuongeza umakini barabarani hasa wakati huu wa kuelekea sikukuu za Krismasi na mwaka mpya ili kuepuka ajali zisizokuwa za lazima.

Kauli hiyo ameitoa mjini hapa leo Alhamisi Desemba 15, 2022 wakati wa mapokezi ya nwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara.
Sagini ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, amesema kuwa uzoefu unaonyesha kuwa kumekuwepo na ajali nyingi hasa nyakati kama za mwisho wa mwaka, zikisababishwa na uzembe wa madereva

“Tunapoelekea kwenye sikukuu hizi niwakumbushe Watanzania wenzangu hasa madereva kuongeza umakini wawapo barabarani tujipange kusherehekea lakini tubaki salama,” amesema.
Sagini ambaye pia ni Mbunge wa Butiama amesema kuwa madereva wengi wamekuwa wakijisahau na kusababisha ajali nyingi zinazosababishia watu ulemavu au vifo.
“Mara nyingi ajali zimekuwa zikiongezeka tunapofika nyakati kama hizi na madhara yake ni makubwa sasa hakuna sababu ya kuendelea na hali hiyo ilhali uwezo wa kuzuia tunao hebu tuongeze umakini zaidi barabarani

 

chanzo mwananchi