BUNDA;Betri za Taa za barabarani Bunda zaibwa Viongozi wa kata na wilaya waapa kukamata wahusika wote
17 November 2022, 9:31 pm
Viongozi wa Kata ya Balili Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara wakerwa na uharibifu wa taa za barabarani unaoendelea kujitokeza katika eneo la Balili.
Wakizungumza na Radio Mazingira Fm kwa nyakati tofauti viongozi hao wamesema baadhi ya wananchi wasiokuwa waaminifu wamekuwa wakiiba betri za Taa za Barabara kuu ya Mwanza-Musoma jambo linalopelekea eneo hilo kurudi gizani.
Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wakazi wa Balili wamesema kutokana na wizi huo umeachanmgia baadhi ya maeneo ya barabara kuwa gizani na kukwamisha shughuli za maendeleo ambazo zinachangiwa na uwepo wa taa hizo
kwa upande wake katibu tawala wilaya Bunda amesema Serikali wilayami bunda itawachukulia hatua kali za kisheria wale wote waliohusika ma wizi wa betri za taa za barababarani eneo la balili wilayani bunda
Kauli hiyo imetolewa na katibu tawala wilaya ya bunda Mhe Salumu Halfani Mterela ofisini kwake ambapo amesema ni jambo la kufedhehesha sana ambapo serikali inaleta maendeleo kwa watu lakini kundi la watu wasio waaminifu wanaihujumu.
Aidha amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika ulinzi wa miundombinu inayoletwa na serikali na pindi wanapobaini mtu anayehujumu miundombinu watoe taarifa kwenye mamlaka