Wananchi wa Kabarimu Bunda waitaka serikali kuondoa dampo karibu na makazi na chanzo Cha maji wakihofia kipindupindu
29 October 2022, 8:49 pm
Wakazi wa kata ya a kabarimu halmashauri ya mji wa bunda Wameitaka serikali kuliondoa dampo la taka lililopo katika mtaa wa saranga mjini Bunda
Wakizungumza katika kikao Cha kata kuhusu Maendeleo kilichitishwa na Diwani wa kata hiyo Mhe Muhunda Nyaimbo Manyonyoryo wananchi hao wamesema dampo hilo kuwepo ni hatari kwa kuwa lipo karibu na kisima Cha maji kinachotumiwa na wakazi wa saranga pili ni karibu na makazi ya watu ambapo kuwepo kwake kunaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa ikiwemo kipindupindu.
Mbali na dampo wananchi hao wameiomba serikali kusambaza mahindi ya bei nafuu katika kila kata lengo ni kuwapunguzia wananchi umbali mrefu wa kuyafata mahindi hayo ambapo wamesema hata wakienda wanakuta foleni ndefu inayopelekea wengine kukosa kutokana na muda kuisha wakati bado hawajahudumiwa
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata Mhe Muhunda Nyaimbo Manyonyoryo amewataka wananchi kuwa na subra pindi viongozi wanashughulikia changamoto zao kwa kuwa wamezichukua likiwemo la Dampo
Aidha ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita tayari imeshaleta zaidi ya shilingi Bilioni 1.2 kata ya kabarimu huku wadau wameshatoa zaidi ya milioni 50 kwa ajili ya maendeleo katika kata hiyo