DC NASSAR: Wafanyabiashara toeni risiti na wateja daini risiti msako kuanza
25 September 2022, 8:50 pm
Mkuu wa Wilaya ya Bunda Jushua Nassar katikati katika semina ya TRA kwa wafanyabiashara
Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Joshua Nassar amesema kuna haja na umuhimu mkubwa kwa wafanyabiashara kujua mabadiriko ya sheria ya Kodi ili kuondoa mkanganyiko baina ya TRA na wafanyabiashara.
Geoffrey Comoro. Afisa elimu na huduma kwa mlipa kodi Mkoa wa Mara
Mhe Nassar ameyasema hayo leo katika semina ya TRA na wafanyabiashara juu ya kuelewa mabadiriko ya sheria ya huku akiwataka wafanyabiashara wazingatie matumizi ya mashine za EFD na wazingatie kutoa risiti za EFD pia kuhakikisha wanalipa kwa wakati wasisubili kusukumana.
Meneja TRA Wilaya ya Bunda Tumain Tinuga
Afisa Kodi Wilaya ya Bunda- Mary Chindongo
Naye meneja wa tra wilaya ya Bunda ndugu Tumaini Tinuga amesema ni kawaida kwa TRA kutoa elimu kwa wafanyabiashara ili kujua mabadiriko ya sheria yta kodi pindi zinapotokea.
Kwa upande wake Jane Mussa mfanyabiashara kutoka Bunda amesema wanaishukuru TRA kwa kuwapa elimu wafanyabiashara katika kujua mabadiriko ya sheria ya kodi ila ameiomba katiaka zoezi la kukadiria mapato ya wafanyabiashara wazingatie na hali halisi ya maisha ilivyo.
By Adelinus Banenwa