Bunda: mapipa 30 ya lami yenye thamani ya zaidi ya milioni 30 yakamatwa yakitoroshwa
24 August 2022, 8:46 pm
Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Joshua Nassar amekamata mapipa 32 ya lami yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 30 za kitanzania katika eneo la kiloleli nyamanguta Halmashauri ya Wilaya ya Bunda
Akiwa kituo Cha polisi Bunda Mhe Nassar amesema hadi sasa wanamshikilia mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi kwa tuhuma hizo.
Amesema ni jambo la kusikitisha sana kuona jambo linafanyika ndani ya kijiji na kuna viongozi hawana habari pia hata wananchi hawatoi taarifa kwa mamlaka
Mhe Nassar ameongeza kuwa vitendo vya wizi kwenye miradi ya maendeleo ndani ya Wilaya ya Bunda havitavumiliwa na kila atakayejaribu kufanya hivyo hakika atakamatwa na hatua Kali zitachukuliwa huku akitoa wito kwa wananchi kuwa na utamaduni wa kutoa taarifa za uhujumu na wizi na uharifu katika maeneo Yao hasa kwenye miradi
Kwa upande wake msimamizi wa miradi wa barabara ya Nyamuswa Bulamba Eng, Liu ZengLang ambapo ndipo inaamini lami hiyo kuibiwa amesema wizi wa vifaa vya miradi ndiyo chanzo Cha miradi kuchelewa pia ni hasara kwa serikali na Kampuni Yao kutokana na hujuma hizo
Bwani Liu amewataka wananchi wanaoishi Kando ya mradi wa barabara ya Nyamuswa – Bulamba kutoa taarifa za wizi pale wanapoona inatoke