Bunda: Ahukumiwa miaka 2 jela kwa kosa la kujeruhi
28 April 2022, 1:18 pm
Mahakama ya wilaya ya Bunda mkoani Mara imemuhukumu kifungo cha miaka 2 gerezani na fidia ya sh. Laki tatu ndugu Maisha Ngoko maarufu kwa jina la Kishosha Ngoko 31 mkazi wa kijiji cha Kihumbu kwa kosa la kumjeruhi kwa kumkata na panga mkononi karibu na Bega na kwenye titi Mariam Willium 24 mkazi wa kihumbu.
Hukumu hiyo imetolewa leo na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bunda mh. MLOKOZI KAMUNTU baada ya kujiridhisha na ushahidi ulitolewa na mashahidi watatu upande wa mhanga na pasipo shaka mstakiwa amekutwa na hatia.
Mwendesha mashtaka wa Serikali Theophil Mazuge akisoma shauri hilo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi amesema mshtakiwa huyo alitenda kosa la kumshambulia na kumjeruhi kwa panga maeneo ya mkononi karibu na bega na kwenye titi Mariam Wilium mnamo tarehe 31mwezi wa kumi mwaka 2021ambapo ni kinyume na kifungu cha 225 cha kanuni ya adhabu sura 16 mapitio ya mwaka 2019
Mshtakiwa ameomba kupunguziwa adhabu kwamadai kuwa yeye anategemewa na familia.
Hata hivyo Mh. Hakimu baada ya kusikiliza maombi ya mshitakiwa kupunguziwa adhabu amemuhukumu kwenda jela miaka 2 kwa mujibu wa kifungu cha 225 cha kanuni ya adhabu sura 16 mapitio ya mwaka 2019.