Mazingira FM
Bunda: waliochukua viuatilifu bila kuwa wakulima wapewa siku Saba kuvirudisha
13 March 2022, 10:32 pm
Balozi wa Pamba nchini Tanzania Mh Agrey Mwanri ametoa wiki Moja kwa watu wote waliochukua viuatilifu vya zao la Pamba bila kuwa na mashamba kuweza kujisalimisha kwa viongozi wa zao la Pamba ngazi ya kata na Wilaya
Ametoa agizo hilo Leo akiwa kata ya Chitengule katika ziara anayoifanya ndani ya Wilaya ya Bunda ambapo ataifanya ndani ya siku tatu.
Balozi huyo wa Pamba nchini amesema wapo watu ambao siyo waaminifu walichukua dawa za Pamba maarufu viuatilifu zaidi ya kiasi Cha mashamba waliyonayo huku wengine hawana mashamba kabisa.
Mh Mwanri amesema kwa wale wote watakaojisalimisha ndani ya wiki Moja wasichukiliwe hatua za kisheria lakini kwa wale wote watakaokaidi agizo hilo baada ya wiki Moja wasimamizi wa zao la Pamba Wilaya wataendesha oparesheni maalumu kuwasaka wale wote waliofanya udanganyifu kwenye uchukuaji wa dawa hizo za Pamba na watahesabika kama wahujumu Uchumi.
Aidha Amemuomba mkuu wa Wilaya ya Bunda kumsaidia kuwakamata na kuwaweka ndani wale wote waliochukua viuatilifu zaidi ya mashamba yao Baada ya hiyo wiki moja
kwa upande wake katibu wa Wilaya ya Bunda Mh Salum Khalifani Mtelela amesema wameyapokea maombi ya balozi wa Pamba Tanzania na amewaelekeza watu wote waliochukua viuatilifu bila kuwa na mashamba kutumia muda uliotolewa kuvisalimisha