Watanzania watakiwa kuwaamini wataalamu wa ndani
3 February 2022, 9:40 am
Wito umetolewa kwa wananchi kuendelea kuwaamini wataalamu wazawa wanaotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao na kuacha kuwabeza
Hayo yamesemwa na mkurugezi wa kampuni ya AUDECIA Investiment Eng Kambarage Wasira anayetekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Guta – Nyabehu yenye urefu wa Kilometa 8 kuelekea lilipo chujio la maji.
Akizungumza na na Mazingira FM ilipofika kuona kazi inavyoendelea Eng Kambarage amesema mitazamo ya watu inasababisha wataalamu wa nyumbani kuonekana hawafai ila ukweli ni kwamba kuna wataalamu wa ndani wana uwezo wana vifaa hasa mainjinia wa barabara kama alivyo yeye na ametekeleza miradi mingi chini ya TARURA
Ametoa wito kwa wananchi na mamlaka kuendelea kushirikiana na wataamu wa ndani ili kuleta maendeleo katika jamii yetu
Insert…………
Ikumbukwe kwamba mradi wa chujio la maji unaojengwa Nyabehu kata ya Guta Halmashauri ya Mji wa Bunda imeghalimu zaidi ya shilling bil 10 ambapo ni moja ya miradi mnne atakayoitembelea Mh Rais Samia Suluhu Hasani atakapofanya ziara ya kiserikali wilayani Bunda Feb 7, 2022