Mpanda FM

MPANDA,Homa ya Ini Yaongezeka kwa Kasi

7 March 2024, 3:09 pm

“Daktari wa Manispaa ya Mpanda  Coronel Bruno amesema kuwa  ongezeko la Ugonjwa huo inatokana na Wananchi kutokuzingatia  kupima Afya kila mara ili kubaini.” Picha na Mtandao.

Na Veronica Mabwile-katavi

Baadhi ya Wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi  wameiomba Serikali mkoani Katavi kuongeza jitihada za utoaji wa Elimu juu ya Magonjwa ya Kuambukiza  ikiwemo  Ugonjwa wa  Homa ya ini ili kuongeza uelewa kwa Wananchi.

Wananchi hao wametoa ombi hilo kufuatia uwepo wa ongezeko  la ugonjwa huo na kusema kuwa  namna ya kutokomeza Ugonjwa huo ni pamoja na Wananchi kupewa elimu ya kutosha juu ya dalili za Ugonjwa huo na namna ya kujikinga.

“Sauti za wananchi wakizungumza kuhusu uelewa wao Juu ya homa ya Ini na hatua gani zichukuliwe ili kukabiliana nao”

Akizungumza  Wakati wa kongamano la Wanawake daktari wa Manispaa ya Mpanda  Coronel Bruno amesema kuwa  ongezeko la Ugonjwa huo inatokana na Wananchi kutokuzingatia  kupima Afya kila mara ili kubaini

“Sauti ya Daktari wa Manispaa ya Mpanda  Coronel Bruno alipokuwa akizungumza katika kongamano la Wanawake kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani kuhusu sababu za kuongezeka kwa ugonjwa huo”

Miongoni mwa dalili za ugonjwa wa homa ya ini ni pamoja na Mcho kubadilika rangi  na kuwa ya Njano,  kupungua Uzito,  hamu ya kula ,pamoja na ngozi ya Mwili kuwasha.