Mpanda FM

Sauti ya Katavi (Matukio)

23 May 2023, 8:02 pm

MPANDA

Wananchi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani hapa Katavi wameshauriwa kubadilisha mfumo wa maisha katika vyakula wanavyokula ikiwa ni pamoja na kujenga desturi ya kufanya mazoezi ili kujiepusha na magonjwa yasiyo ya kuambukiza

Dr Paulo Swakala ambaye ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mpanda amesema idadi ya wagonjwa wa magonjwa hayo yasio ya kuambukiza yanaongezeka kuliko magonjwa ya kuambukiza VERONICA MABWILE ametembelea ofisi ya mganga mkuu manispaa ya mpanda na kutuandalia taarifa hiyo.

KATAVI

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imefanikiwa kufichua maduka yanayouza viuatilifu ambavyo ni mali ya serikali chini ya usimamizi wa bodi ya pamba.

Haya amebainisha Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi Faustine Maijo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya TAKUKURU katika robo ya Januari hadi Machi 2023 mbele ya waandishi wa Habari amebainisha kuwa maduka 5 yamebainika yanauza viuatilifu aina ya Bodigadi 500 WDG,

JOHN BENJAMIN ana undani wa taarifa hii.

MPANDA

Jamii imeshauriwa kufanya usafi wa kinywa kwa kuzingatia muda na kuepuka matumizi holela ya  dawa zisizo za kitabibu ili kuepukana na magonjwa ya kinywa na meno.

Ushauri huo umetolewa na daktari wa meno Kelvin Mremi kutoka hospitali ya manispaa ya Mpanda wakati akizungumza na Mpanda Radio fm undani wa taarifa hii anatuletea KINYOGOTO FESTO.

ARUSHA   -KATAVI

Inaelezwa kuwa kumekuwa na vitendo vya ukiukaji wa haki za Wanyama huku wafugaji wengine wakionyesha kutozitambua haki hizo za Wanyama.

Hayo yamejiri baada ya  mwandishi wa habari  dotto kadoshi kutokea jijini Arusha kuwa mbogo na kujikuta akisimamisha gari ya abiria inayofanya safari zake kutoka Arusha kwenda Moshi mara baada ya kuona kuku waliobebwa katika gari hiyo ya abiria na kuwataka kusitisha safari yao mpaka pale watakapowaweka katika mazingira mazuri kuku hao, Huyu hapa  anna millanzi anakujia na undani wa taarifa hii huku akiwa amefanya mahojiano na wafanyabiashara wa kuku mkoani hapa ili kutambua wanazifahamu haki za Wanyama na wanazifuata?.

MICHEZO

Kesho Tiger fc na Malimao FC kuminyana katika mechi ya kirafiki wakati KMC wakijinoa kuelekea mechi 2 za mwisho na kimataifa fainali za NBA pale Marekani zaendelea.

Mwanamichezo wetu Killian Samwel anakuja na utondoti wa taarifa hizo.