Mpanda FM

Askari wa zimamoto Katavi washauriwa kufanya kazi kwa weledi

20 December 2023, 5:15 pm

Askari wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji Katavi washauriwa kufanya kazi kwa weredi na kuendelea kuwa wavumilivu.

Na Gladness Richard – Katavi

Askari wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji mkoani Katavi wameshauriwa kufanya kazi kwa weredi na kuendelea kuwa wavumilivu pindi wanapokutana na changamoto kazini.

Kuwataka kuwa waadilifu katika kutekeleza majukumu ili   waweze kulitumikia taifa kwa utiifu kwa mujibu wa viapo vyao.

Ushauri huo umetolewa na Kamanda mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji kamishina msaidizi Regina Paul Kaombwe   Na kuwataka kuwa waadilifu katika kutekeleza majukumu ili   waweze kulitumikia taifa kwa utiifu kwa mujibu wa viapo vyao.

Sauti ya Regina Kaombwe

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Busweru aliyekuwa mgeni Rasmi akimwakilisha mkuu wa mkoa Mwanamvua Mrindoko amempongeza Kamishina Regina kwa utendaji wake mahiri wa kazi ndani na jeshi la zimamoto uokoaji aliyemaliza utumishi wake mkoani Katavi.

Sauti ya Onesmo Buswelu

Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji  mkoa wa Katavi Geofrey Mwambungu kwa  niaba ya Askari wote wa jeshi hilo amesema kuwa licha ya kuwa ni Kamishina vilevile  amesimama kama  mama mlezi  na kumwomba watakapo pata changamoto katika upande wa kazi asisite kuwaonyesha ushirikiano.

Sauti ya Geofrey Mwambungu