Mpanda FM

Kapufi afanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

15 December 2023, 3:59 pm

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi akiwa ziarani. Picha na Maktaba

Mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Sebastiani Kapufi afanya ziara kukagua miradi ya maendeleo iliyopo katika jimbo lake.

Na Deus Daud – Mpanda

Mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Sebastiani Kapufi amefanya ziara kukagua miradi ya maendeleo iliyopo katika jimbo lake ili kufanya tathimini ya ukamilishwaji wa miradi hiyo

akizungumza Kapufi wakati akikagua majengo ya hospitali ya manispaa ya Mpanda amesema kuwa mfuko wa jimbo la  utachangia shilingi milioni 6 ili kukamilisha ujenzi wa majengo muhimu katika hospitali hiyo.

Sauti ya Sebastian Kapufi

kwa upande wao wananchi  wakizungumza wakati wa ziara hiyo wameipongeza serikali kwa kukamilisha miradi ikiwemo  ya  sekta ya elimu na afya na kumwomba mbunge kuongeza nguvu ya fedha ili waweze kukamilisha miradi waliyoanza kujenga kwa nguvu za wananchi.

Sauti ya Wananchi

miongoni mwa miradi iliyotembelewa katika siku ya pili ya kuhitimisha ziara ni  Pamoja na hospitali ya manispaa ya Mpanda , kituo cha afya cha Nsemurwa , shule ya msingi Kawajense.