Mpanda FM

Diwani Wense akaribisha wawekezaji kukuza uchumi

22 April 2026, 2:18 pm

Wense Kamtoni diwani wa kata ya kashaulili. Picha na John Benjamin

“Biashara hii imeanzishwa kwa lengo la kutoa huduma kwa jamii na kukuza uchumi”

Na John Benjamin

Wawekezaji wameombwa kujitokeza kuwekeza katika nyanja ya kibiashara kata ya kashaulili iliyopo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi

Hayo yamebainishwa na diwani wa kata ya kashaulili Wense Kamtoni katika ufunguzi wa Hela Supermarket iliyopo mtaa wa Simba ambapo ameeleza kuwa uwekezaji huo ni moja ya nyanja ya kukuza uchumi na kuahidi kuwaunga mkono wawekezaji

Sauti ya diwani

Kwa upande wake mmiliki wa Supermarket hiyo Herymathew Raymond amewakaribisha wananchi kufika na kupata huduma katika Supermarket hiyo huku akiahidi  kutoa huduma bora Kwa wateja wataofika katika duka hilo

Sauti ya mmiliki

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliofika kushuhudia uzinduzi huo wamesema kuwa uwekezaji unaoendelea kuwekezwa katika mkoa wa Katavi umekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo na   wamempongeza mwekezaji huyo Kwa uwekezaji katika eneo hilo.

Sauti za wananchi

Uwekezaji katika maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wa Katavi inatajwa kuwa moja ya jambo linalosaidia kukuza uchumi.