Mpanda FM

KATAVI, Miti Milioni Kumi Kupandwa Kutunza Mazingira.

1 February 2024, 3:02 pm

Halmashauri zote zilizopo mkoani Katavi kuhakikisha zinapanda miti milioni 2. Picha na Festo kinyogoto

Na John Benjamin-katavi

Halmashauri zote na mamlaka za Mistu  mkoani Katavi zimetakiwa kuhakikisha zinapanda Miti  kwa ajili ya kutunza mazingira na uoto wa AsiliHayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko katika hafla ya uzinduzi wa wiki ya Mazingira ambapo amesema kuwa kila Halmashauri zote zilizopo mkoani Katavi kuhakikisha zinapanda miti milioni 2 ambapo milioni moja na laki tano ni miti kwaajili ya Uoto wa asili na laki tano kwaajili ya Matunda.

Sauti Ya Mkuu wa Mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumzia uzinduzi wa zoezi la kupanda miti.

Akizungumza kwa niaba ya wakurugenzi  Halmashuri 5 zilizopo mkoani hapa Katavi mkurungezi mtendaji wa halmashuri ya Nsimbo Mohamed Ramadhani amesema wamepokea maelekezo hayo ambapo kwa upande wa halmashuri ya Nsimbo imekwisha anza kutekelezaji wa maagizo hayo.

Sauti ya ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Nsimbo Mohamed Ramadhani akizungumzia zoezi hilo la upandaji Miti.

Malengo la zoezi hilo la upandaji miti ni kutunza mazingira na Mkoa wa Katavi kufika mwezi March mwaka huu unatarajiwa kupanda miti milioni 10.