Mpanda FM

Mrindoko Aahidi Malipo ya Tumbaku

6 September 2023, 10:15 am

KATAVI

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewahakikishia malipo zaidi ya Dola Milioni 2.5 wakulima wa zao la Tumbaku katika msimu wa kilimo 2022/2023 wa Amcos 6 zilizoingia Mkataba wa ununuzi wa Tumbaku na Kampuni ya Mkwawa Leaf LTD.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari RC Mrindoko amesema kuanzia tarehe 4 septemba na wataanza kulipwa na amezitaja Amcos sita ambazo hazijalipwa fedha zao na Kampuni ya Mkwawa kuwa ni Nsimbo , Bulamata ,Magunga ,Kasekese , Muungano na Ilunde.

Mrindoko amesema Jumla ya fedha ambazo wakulima wa Amcos hizo wanazodai Kampuni ya Mkwawa ni Dola za Kimarekani Milioni 2.582 Huku Akisema tatizo la wakulima kutolipwa fedha zao kwa wakati si Mkoa wa Katavi peke yake na limetokana na matatizo ya kiuchumi duniani ulisababishwa na uhaba wa Dola .

Katika hatua Nyingine amewaelekeza wakuu wa Wilaya wote wa Wilaya zilizopo katika Mkoa wa Katavi kusimamia fedha hizo mara baada ya kuwa zimeingia kwenye Akaunti za Amcos wahakikishe wakulima wanalipwa malipo kwa haraka pasipokuwa na kucheleshwa .

#mpandaradiofm97.0

#amcos