Mpanda FM

CCM wilaya Mpanda yaingilia uchaguzi wa shina ulioshindikana mara mbili

19 February 2024, 4:32 pm

Picha na Samwel Mbugi

Wamesimamia uchanguzi na kumpata mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa shina la Mpanda Hotel Donard Chrispin Mpazi aliyeshinda kwa kupata kura 195 kati ya wapiga kura 326 baadaya uchaguzi huo kushindwa kufanyika mra mbili.

Na Samweli Mbugi-Katavi

Chama cha Mapinduzi CCM Shina la Mpanda Hotel Manispaa ya Mapanda Mkoa wa Katavi kimefanya uchanguzi wa mwenyekiti wa Shina February 17, 2024.

Uchanguzi huo umesimamiwa na Vingozi kutoka  Ngazi ya Wilaya  Masud Mary Mary  na Gilbart Kaswiza ambao wamesimamia uchanguzi na kumpata mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa shina la Mpanda Hotel Donard Chrispin Mpazi aliyeshinda kwa kupata kura 195 kati ya wapiga kura 326 baadaya uchaguzi huo kushindwa kufanyika mra mbili.

Sauti ya Masud Marry marry akitangaza matokeo ya uchaguzi.

Baada ya matokeo Wagombea walioshiriki uchaguzi huo wamesema uchanguzi huo ulikuwa wa haki na amani, ambapo wamewashukuru wapiga kula wao kwa kuwapigia kula walizopata kwani chaguzi za awali zilikuwa zimegubikwa na makundi ya ndani ya Chama.

Sauti ya wagombea

Mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Shina  Donald Pazi ametoa shukrani kwa wapiga kula wote waliojitokeza kwenye uchaguzi huo ambao umefanyika kwa amani tofauti na chaguzi mbili zilizopita kuharibika bila kumpata mshindi huku akiahidi kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.

Sauti ya mwenyekiti mpya wa Shina Donald Pazi

Wanachama cha Mapindunzi CCM waliohudhulia kupiga kula wamesema uchaguzi huo umefanyika vizuri bila upendeleo wowote tofauti na chaguzi zilizopita kipindi cha nyuma kwakuwa wasimiamizi walitaka kupitisha wagombea bila kutenda haki.

Sauti za wanachama wa Ccm waliopiga kura

Wanachama wa Ccm waliopiga kura

Hata hivyo Mpanda Radio imezungumza na Msimamizi  Glibart Kaswiza Mjumbe wa kamati ya siasa Wilaya amesema wao wamekuja kusimamia uchaguzi huo baada ya kuona kuwa chaguzi mbili kuharibika bila mafanikio ya kumpata mwenyekiti wa shina.

Msimamizi wa uchaguzi huo Masud Mary Mary Mjumbe wa kamati ya siasa Wilaya  amemtangaza Donard Pazi kuwa mshindi kati ya wagombea watatu, ambapo mgombea wa pili Rehema Miraji Kisunga amepata kula 106 na mgombea wa tatu Doto Festo Ndege Ulaya amepata kula 9.