Mpanda FM

Wananchi Tanganyika Waomba Elimu ya Afya ya Meno na Kinywa

30 March 2023, 3:38 pm

KATAVI

Baadhi ya wananchi wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wameomba kupatiwa elimu ya afya ya kinywa na meno kabla ya kupata athari.

Wakizungumza na Mpanda radio Fm wamekiri kupata huduma bora ya afya ya meno huku wakiomba serikali kutoa elimu juu ya afya ya meno.

Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Tanganyika Erick Maziara amesema wameshaanza utaratibu wa kutoa elimu kupitia shule za msingi na ambapo wapo katika mchakato wa kutoa taarifa kwa shule pamoja na wazazi.