Mpanda FM

Katavi: Wachimbaji waaswa kuchukua tahadhari migodini kipindi cha mvua

1 February 2024, 5:54 pm

Kaimu kamanda  Geofrey Mwambungu  amesema kuwa kuna ajali nyingi hutokea katika maeneo ya Migodini  kipindi cha mvua”. Picha na Gladness Richard.

Na Gladness Richard-Katavi

Wachimba wa madini mkoani Katavi wameshauliwa kuchukua tahadhali kabla hawajaingia kwenye Migodi  katika kipindi hiki cha mvua ili wasidondokewe na kifusi.

Ushauli huo umetolewa na Mkaguzi wa Jeshi la  zimamoto na uokoaji  mkoa wa Katavi kaimu kamanda  Geofrey Mwambungu  amesema kuwa kuna ajali nyingi hutokea katika maeneo ya Migodini  kwani mvua zinaponyesha husababisha kuta za udongo hurainika na kusababisha kuanguka kwa migodi.

Sauti ya Mkaguzi wa Jeshi la  zimamoto na uokoaji  mkoa wa Katavi kaimu kamanda  Geofrey Mwambungu akitoa tahadhari kwa wachimbaji kuchukua tahadhari kipinddi cha mvua wanapokuwa Migodini

Kwa upande wao wachimbaji wa madini wamesema kuwa wanatumia mbinu mbalimbali kwa kufunga Kamba pindi wawapo kuwa  Mashimoni na kuvaa kofia Ngumu.

Sauti ya Wachimbaji wakieleza juu ya tahadhari wanazochukua wanapokuwa Migodini.

Mwambungu ameongezea kwa kusema kuwa ni jukumu lao  kama Jeshi la zimamoto na uwokoaji kuwasimamia, kuwakagua na kuhakikisha wachimbaji wanakuwa salama wakati  waingiapo migodini.