Mpanda FM

Ufinyu ardhi ya kilimo kilio Nsimbo

24 July 2023, 10:24 am

NSIMBO

Wananchi wa kijiji cha Usense kata ya Uruwila halmashauri ya Nsimbo wamepaza sauti zao juu ya ufinyu wa maeneo ya kufanya shughuli za kilimo.

Hayo wameyasema wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Nsimbo Anna Lupembe katika kata ya Uruwila wamesema kutokana na ongezeko la watu wananchi wanashindwa kufanya shughuli za kilimo Kwa kiwango kikubwa huku wakiomba kuongezewa eneo kutoka kwa Wakala wa Misitu Tanzania [TFS].

Kwa upande wake mbunge wa Jimbo La Nsimbo Ana Lupembe amesema atazungumza na wakala wa uhifadhi wa misitu Ili kutoa nafasi Kwa wakulima hao kufanya shughuli zao.

Mbunge Ana Lupembe bado anaendelea kufanya ziara katika kata zote kwenye Jimbo lake la Nsimbo.

#mpandaradiofm97.0

#tfs