Mpanda FM

Katavi: Agizo la RC upatikanaji maji soko la matunda lapuuzwa

7 June 2023, 10:19 am

MPANDA

Ikiwa saa 24 zimepita baada ya agizo la kupatikana maji Soko la Matunda lililopo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wafanyabiashara wameomba uongozi wa mkoa kufuatilia kwa kina upatikanaji wa maji sokoni hapo.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio Fm na kuongeza kuwa bomba hilo hushinda limefungwa licha ya agizo lililotolewa na mkuu wa mkoa wa Katavi juu ya upatikanaji wa maji sokoni hapo.

Ikumbukwe mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko alipopita sokoni hapo Mei 30 alitoa agizo kuwa ndani ya saa 24 maji yaanze kutoka sokoni hapo.

Licha ya changamoto hiyo ya maji soko hilo linakabiliwa na changamoto ya choo ambacho si rafiki kwa eneo hilo la soko.

#mpandaradiofm97.0

#katavists

#wizarayamaji