Mpanda FM

RC Katavi ashauri kubadilishwa mkandarasi barabara ya Kibaoni-Stalike

15 January 2024, 11:39 am

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko( upande wa kulia)akitoa Maelekezo baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa Barabara.Picha na Kinyogoto Festo

Barabara hiyo imekuwa na changamoto Kwa muda mrefu Kwani Wananchi wanapata adha ya kusafiri Kwa muda wa masaa manne Kwa kilometa 70

Na Kinyogoto Festo-Katavi

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ameshauri kubadilishwa Mkandarasi anaejenga Barabara ya Kibaoni hadi Stalike kutokana kusuasua kwa ujenzi huo .

Mwanamvua ameyasema hayo kufuatia taarifa ya ujenzi wa Barabara hiyo iliyobainisha kuchelewa kutekelezwa kwa mradi huo na ameshauri kubadilishwa Mkandarasi kwakuwa malipo yote yametolewa lakini utendaji wa kazi umekuwa nyuma ya Matarajio ya Miezi 36 ambayo mpaka sasa ni asilimia 13 pekee Ya kazi iliyofanyika Kwa Miaka Miwili.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindiko akieleza kuhusu kubadilishwa Mkandarasi

Jovin Ndiyetabula Mhandisi msimamizi mkazi amesema changamoto Kwa sasa ni hali ya hewa ambayo inazuia utendaji wa baadhi ya kazi ambapo Kwa sasa kazi zinazoendelea ni ujenzi wa Kalavati na usafishaji licha ya kwamba malipo yalifanyika Mapema Mhandisi  amesema  utendaji wa Mkandarasi bado ni wa kusuasua

Sauti ya Jovin Ndiyetabula Mhandisi Msimamizi Mkazi akieleza kuhusu hali ya ujenzi wa barabara hiyo

Mhandishi Jovin Ndiyetabula wa kwanza kushoto akieleza kuhusu mradi huo wa Barabara.Picha na Kinyogoto Festo

Aidha Mwanamvua amesema Barabara hiyo imekuwa na changamoto Kwa muda mrefu Kwani Wananchi wanapata adha ya kusafiri Kwa muda wa masaa manne Kwa kilometa 70 hivyo hajaridhishwa na amesema ni uzembe kwani tangu mwaka 2022 bado kazi si yakulidhisha.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi akizungumza kuhusu barabara hiyo na adha wanayoipata Wananchi

Kukamilika kwa ujenzi huo wa Barabara ya Lami yenye urefu wa Kilometa 73 kutoka Mpimbwe hadi Stalike unatarajia kutatua adha ya kutembea muda mrefu na kufungua zaidi halmashauri hiyo katika fursa za Kilimo.