Mpanda FM

Wananchi Ugala waiomba serikali kutolea ufafanuzi wa maeneo wanayoishi

10 November 2023, 1:58 pm

Picha na Mtandao

Wananchi wa Kijiji cha Kimani kata ya Ugala halmashauri ya Nsimbo wameiomba serikali kutolea ufafanuzi malalamiko ambayo yanawataka kuhama.

Nsimbo

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kimani kata ya Ugala halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wameiomba serikali kutolea ufafanuzi juu ya malalamiko ambayo yanawataka kuhama katika maeneo wanayoishi.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara mbele ya Mkuu wa wilaya ya Mpanda wananchi hao wamesema wamekuwa wakiambiwa kuhama katika maeneo yao ambayo yanadaiwa kuwa hifadhi ya msitu.

Sauti ya Wananchi

Mohamed Ramadhani ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Nsimbo amesema eneo hilo linatambulika kuwa ni hifadhi ya msitu huku akiendelea kuwaasa wananchi hao kuwa na subra wakati jambo hilo likitafutiwa ufumbuzi.

Sauti ya Mohamed Ramadhani

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amewataka wananchi kuondoka katika maeneo hayo ya hifadhi ya misitu huku akisisitiza sheria ya msitu kutumika kwa wale wote waharibifu wa miti watakao kiuka sheria hiyo.

Sauti ya Jamila Yusuph