Mpanda FM

MPANDA, Madiwani Wahofia Bajeti Ya TARURA

7 March 2024, 2:31 pm

“Madiwani Wa Halmashauri ya Manispaa Ya Mpanda Wameonyesha Kutoridhishwa Na Bajeti Hiyo Na Kumtaka Manager Wa Tarura Kwenda Kupitia Upya Na Kuiwasilisha Kwa Baraza Hilo Ifikapo Jumatatu ya tarehe 11 mwezi wa tatu mwaka huu” Picha na Deus Daud

Na Deus Daud-katavi

Baraza La Madiwani Manispaa Ya Mpanda Mkoani Katavi Limepitisha Mapendekezo ya Bajeti Ya TARURA Ya Shilingi Billioni 4.8, Ambayo Itakwenda Kurekebisha Barabara Zilizpo Manispaa Ya Mpanda Mkopani Hapa.

Katika Kikao Hicho Madiwani Wa Manispaa Ya Mpanda Wameonyesha Kutoridhishwa Na Bajeti Hiyo Na Kumtaka Manager Wa Tarura Kwenda Kupitia Upya Na Kuiwasilisha Kwa Baraza Hilo Ifikapo Jumatatu ya tarehe 11 mwezi wa tatu mwaka huu.

Sauti ya Madiwani wakati wakitoa hoja kwenye baraza kuhusu ubovu wa miundombinu Manispaa ya MPANDA na bajeti iliyowekwa”

Kwa Upande Wake Manager Wa TARURA Manispaa Ya Mpanda Injinia SIMONI MUNGE amesema Kuwa Watakwenda Kuyafanyia Kazi Maelekezo Waliyopewa na Baraza La Madiwani Ili Kuondoa Changamoto Ya Barabara Iliyopo Manispaa ya Mpanda.

Sauti ya Manager Wa TARURA Manispaa Ya Mpanda Injinia SIMONI MUNGE akieleza jinsi anakwenda kuyafanyia kazi maoni ya Madiwani hao

Aidha Mbunge Wa Jimbo La Mpanda Sebastiani Kapufi Amewataka Madiwani Kuwa Watulivu Kwenye Kipindi Hiki Na Kuitaka TARURA Kuendelea Kushughulikia Maeneo Korofi Yaliyo haribika.

Madiwani walipokuwa wakipitia taarifa ya Mapendekezo ya bajeti. Picha na Deus Daud