Mpanda FM

Mkoa wa Katavi  umepokea  Fedha  zaidi ya Trillion Moja  kutoka kwa Serikali

8 April 2024, 3:07 pm

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko .Picha na Mtandao

Mafanikio ya Mkoa wa Katavi kwa miaka Mitatu ya Serikali ya awamu ya Sita chini ya  Rais Dkt Samia

Na Liliani Vicent -Katavi

Mkoa wa Katavi  umepokea  Fedha  zaidi ya Tshs Trillion Moja  kutoka kwa Serikali ya awamu ya  Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuboresha huduma  za Kijamii na kutatua Kero za Wananchi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko wakati wa Kongamano kuhusu Mafanikio ya mkoa wa Katavi kwa Miaka Mitatu ya Serikali ya awamu ya Sita chini ya  Rais Dkt Samia.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza katika kungamano hilo

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu  amesema  kupitia Fedha zilizotolewa na Serikali Wananchi   wameweza kupata Mradi wa Maji na kutatua Kero iliyokuwa imedumu kwa Muda Mrefu.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu

Nao Baadhi ya Wananchi walioudhuria kongamano hilo wamesema katika Miaka Mitatu ya Serikali  ya awamu ya Sita wameona Mafanikio yaliyofanyika katika Sekta Mbalimbali .

Sauti za Wananchi waliohudhuria kongamano hilo wakitoa shukrani zao kwa mafaniko katika kipindi cha Miaka mitatu ya Uongozi wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia suluhu Hassain