Mpanda FM

Mpanda: Mwanafunzi atekwa, polisi yawadaka watuhumiwa

30 June 2023, 10:17 am

KATAVI

Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi kwa kutuhuma za kumteka mtoto mdogo wa kike (9) mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Mizengo Pinda katika manispaa ya Mpanda.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amewataja watuhumiwa hao waliokamatwa kuhusika na tukio hili kuwa ni Joseph John (24) Yusuph Sadick (27) wakazi wa Mtaa wa Milupwa , Abrahamu Kassim(28) Mkazi wa Mtaa wa Misunkumilo Manispaa ya Mpanda na Samwel Nzobe (41) Mkazi wa Mtaa wa Kotasi Manispaa ya Mpanda ambapo amebainisha kuwa tukio hilo la kikatili la kumteka mtoto huyo lilitokea June 13 majira ya saa nane mchana katika Manispaa ya Mpanda wakati mtoto huyo alipokuwa akitokea shule ambayo anayosoma ya Mizengo Pinda alikukuwa amekwenda kufanya usafi ambapo watuhumiwa walimteka na kutishia kumuua kwa madai vinginevyo walipwe Milioni 50 ili wamwachie ..

Aidha Ngonyani Amesema watuhumiwa hao wote wanne wamekamatwa kufuatia msako mkali ulifanywa na jeshi la Polisi usiku na mchana kufatilia tukio hilo ambapo jeshi hilo la polisi limefanikiwa kumpata mtoto huyo akiwa amefungiwa na watuhumiwa hao ndani ya chumba kwa zaidi ya siku moja

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani Amesema watuhumiwa wote wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi juu ya tukio hili na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo wakabili.

#mpandaradiofm97.0

#jeshilapolisi