Mpanda FM

Polisi Katavi wapambana na vitendo vya ukatili kwa watoto

10 October 2025, 6:43 am

Afande John Mwaipungu akitoa elimu kwa waumini wa KKKT Mpanda. Picha na John Benjamin

“Lengo ni kuwapenda watoto na kuwajali katika Bwana”

Na John Benjamin

Jamii mkoani Katavi imesisitizwa kutambua haki za watoto na kuhakikisha kuwa wanalelewa katika mazingira salama yenye heshima na upendo

Hayo yamebainishwa na mrakibu na Afisa wa jeshi la polisi jamii mkoa wa Katavi John Mwaipungu katika siku ya Mikaeli na watoto iliadhimishwa katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) lililopo Mpanda ambapo ameeleza aina mbalimbali za ukatili wanaofanyiwa watoto ikiwa ni pamoja na ukatili wa kimwili.

Sauti ya afisa wa jeshi la polisi

Kwa upande wao baadhi ya waumini wa kanisa hilo wameshukuru kwa elimu waliyopatiwa na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuacha mara moja tabia ya kuwatumikisha watoto katika shughuli za biashara badala yake wawape nafasi ya kupata elimu na kufurahia utoto wao

Sauti za waumini

Utoaji wa elimu hiyo ni sehemu ya kampeni ya Jeshi la polisi Jamii katika kupambana na vitendo vya kikatili dhidi ya watoto mkoani Katavi.