Mpanda FM

Mwanafunzi kidato cha pili abakwa Katavi

16 June 2023, 7:15 pm

MPANDA

Mwanafunzi wa kidato cha pili mkazi wa Misengereni kata ya Ilembo mKoani Katavi amebakwa na mwanaume ambaye aliingia ndani ya nyumba kwa kuruka ukuta wakiwa wamelala .

Mama mdogo wa binti huyo ameeleza namna tukio hilo lilivyokuwa mara baada ya kuvamiwa na kijana huyo huku akieleza kuwa kijana huyo aliingia na kudai fedha ambazo hakufanikiwa kuzipata na ndipo akafanya tukio hilo la ubakaji mbele yao.

Mwenyekiti wa mtaa huo ameeleza kutokuwa na taarifa juu ya tukio hilo huku akiwataka wananchi kutoa taarifa pindi wanapopatwa na changamoto na kuwataka wananchi kujitokeza kwenye mikutano ili waweze kujadili kwa pamoja masuala ya ulinzi shirikishi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kamishna Msaidizi wa Polisi KASTER NGONYANI amethibitisha kutokea kwa tukio hilo .

Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano na utambuzi zaidi kufuatia tukio hilo.

#mpandaradiofm97.0

#jeshilapolisi