Mpanda FM

Wananchi 53 Mpanda Wanufaika na Mafunzo ya Ujasiriamali

27 April 2023, 8:19 am

MPANDA

Jumla ya wananchi 53 manispaa ya Mpanda mkoani katavi ikiwamo wanawake pamoja na vijana wamenufaika na mafunzo ya ujasiliamali yaliyowezeshwa na Diwani wa viti maalumu kata ya majengo kupitia chama cha mapinduzi CCM lengo likiwa ni kuwapa ujuzi na kuwaondoa katika utegemezi.

Akisoma risala Johannes James amesema wamejifunza namna ya kutengeneza vitu mbalimbali na kueleza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuwainua kiuchumi .

Diwani wa viti Maalumu Kata ya Majengo Kartas Mangwangwa amesema ana imani na darasa hilo ambalo limepata mafunzo kuwa watafanya vizuri katika kile walichojifunza huku akiahidi kuendelea kuwafuatilia wahitimu hao ili waweze kuyafikia malengo yao.

Mgeni rasmi katika Hafla hiyo ambaye ni afisa Tarafa Kashaulili Mboni Mpaye amewataka waliopata mafunzo hayo kuyatumia vizuri mafunzo hayo na kuwataka kujitahidi kutatua changamoto zinazojitokeza ambazo zinaweza kutatulika ili wafikie malengo.