Mpanda FM

Nyumba 50 Zaharibiwa na Mvua Mwamkulu

8 February 2023, 12:30 pm

MPANDA

Nyumba 50 Zimeharibiwa huku kaya 47 zikikosa makazi katika kata ya Mwamkulu Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Kufuatia Mvua iliyonyesha January 31 ,2023

Wakizungumza na Mpanda redio FM Wahanga wa tukio hilo wamesema kuwa mvua hiyo imeleta uharibifu mkubwa wa makazi yao na hasara ya mali zao .

Diwani wa kata ya Mwamkulu Kalipi Katani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema chanzo ni mvua kubwa iliyonyesha hali iliyopekelea uharibifu huo kwa wananchi na barabara kushindwa kupitika kutokana na kufungwa na miti iliyoangukia barabarani huku akiiomba serikali kutoa msaada wa haraka kwa wananchi waliokutwa na maafa hayo.

Aidha diwani wa kata ya Mwamkulu amewaomba wananchi kupanda miti katika maeneo yao na kujenga nyumba bora kwa kufuata sheria za ujenzi ili kuepukana na majanga yatokanayo na mvua.