Mpanda FM

RUWASA kuja na mfumo wa kudhibiti upotevu wa mapato

8 November 2023, 3:07 pm


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Charles Halawa akizungumnza na wajumbe wa kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Nsimbo. Picha na maktaba

Baraza la madiwani Nsimbo Mkoa wa Katavi waishauri Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini [RUWASA]  kuthibiti Mapato.

Na Betord Chove-Nsimbo

Baraza la madiwani katika halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi wameishauri Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini [RUWASA]  kudhibiti mapato  yanayokusanywa na jumuiya za watumiaji maji vijijini ili kuendeleza miradi mingine.

Hoja hiyo imebuliwa na madiwani  katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kinajadili taarifa za taasisi,na Kata kwenye Halmashauri hiyo ambapo madiwani walibainisha upotevu wa mapato pia mafundi wengi wanaotumika na Ruwasa kutokuwa na uwezo wa kuwahudumia wananchi ipasavyo.

Sauti ya Madiwani

Christian Mpena Meneja wa Ruwasa wilaya ya Mpanda  amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na amesema serikali kwa kutambua hilo wameleta watalaamu kwa ajili ya  kutatua changamoto hiyo ya upotevu wa mapato hayo yanayokusanywa.

Sauti ya Christian Mpena

Katika Hatua nyingine  Mpena amesema kuwa watakwenda kutekeleza mradi wa kubadilisha Pampu za mkono kwenye kwenye visima kijiji cha Masewela,Filimule’ Kabulonge,

Sauti ya Christian Mpena