Mpanda FM

Kapufi aahidi kushughulikia mgogoro bwawa la Milala

9 August 2023, 7:13 am

MPANDA

Baadhi ya wakazi wa kata ya Minsukumilo ambao walipisha kufanya shughuli za uzalishaji pembezoni mwa bwawa la milala wameomba kupata hatma yao mara baada ya kupisha uendelezaji.

Wameyasema hayo wakati wa ziara ya mbunge wa Jimbo la Mpanda mjini Sebastian Kapufi wamesema ni muda mrefu tangu tume ya mawaziri ilivofika na kutoa maagizo kutokuendeleza maeneo ya karibu na bwawa la milala huku wakiomba kujua hatma ya maeneo Yao na Mali zao.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo baada ya kupokea kero hiyo amekiri kuibeba na kuipeleka kwa wahusika ili wananchi hao waendelee na shughuli zao za uzalishaji mali ama kulipwa fidia ya mali zao.

Kapufi ameanza ziara ya kuzungumza na wananchi wa jimbo lake August 2 mwaka huu.

#mpandaradiofm97.0

#ccmtanzania