Mpanda FM

English Medium ya serikali kujengwa Mpanda

24 July 2023, 10:20 am

MPANDA

Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi inatekeleza mradi wa ujenzi wa shule ya mchepuo wa kiingereza kwa ajili ya kuwasaidia wazazi na walezi ambao wana nia ya kusomesha watoto kwenye shule binafsi lakini wameshindwa kumudu gharama kubwa za kusomesha.

Ujenzi wa mradi wa shule hiyo unatekelezwa katika eneo la shule ya msingi Misukumilo kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya manispaa ya Mpanda ambapo fedha Mil 260 zinatumika kukamilisha mradi huo.

Haidary Sumry Msitahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda akiongozana na madiwani wote kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa miradi ya maendeleo amesema kuwa shule hiyo itakuwa na kiwango cha juu cha utoaji elimu ya msingi ikizingatiwa ni mali ya serikali.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa shule hiyo Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Misukumilo,Festo Malekela amesema kuwa ujenzi wa mradi wa shule ya mchepuo wa kiingereza unahusisha vyumba nane vya madarasa,ofisi mbili za walimu,matundu 12 ya vyoo na jiko kwa thamani ya Mil 260 ambapo umefikia asilimia 85.

#mpandaradiofm97.0

#WizaraYaElimu