Mpanda FM

Mpanda, Watoto Yatima na Mazingira Maalumu Waguswa na Msaada

7 March 2024, 2:53 pm

“Matendo hayo ya huruma yamefanyika katika shule ya Msingi Nyerere na katika kituo cha kulelea Watoto yatima cha Yohana Paul wa pili Matumaini ya Watoto ambapo wamegawa mahitaji kama vile Madaftari , Mchele, na Juice” Picha na Lillian Vicent

Na Lilian Vicent-katavi

Kuelekea Maadhimisho ya siku ya Wanawake Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Sophia Kumbuli amewaongoza Wanawake kufanya matendo ya huruma kwa Wtoto wa Eimu maalumu pamoja na Watoto yatima

Matendo hayo ya huruma yamefanyika katika shule ya Msingi Nyerere na katika kituo cha kulelea Watoto yatima cha Yohana Paul wa pili Matumaini ya Watoto ambapo wamegawa mahitaji kama vile Madaftari , Mchele, na Juice .

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bi Sophia Kumbuli Akizungumza kuhusu matendo hayo ya huruma

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Nyerere Zuhura Kapama pamoja na Afisa Elimu maalumu wa Manispaa ya Mpanda Anna Sawasawa ametaka wazazi kuendelea kujitoa na kuwaibua watoto wenye ulemavu.

“Sauti ya Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Nyerere Zuhura Kapama pamoja na Afisa Elimu maalumu wa Manispaa ya Mpanda Anna Sawasawa”

Nae mlezi wa kituo cha watoto Yatima Sista Rose Sungura amesema wanaojitokeza kusaidia watoto wanafanya hivyo kwa kuwa wanakujua wamewekeza kwa watoto hao.

“Sauti ya mlezi wa kituo cha watoto Yatima Sista Rose Sungura akitoa shukrani kwa wanawake hao na kuona umuhimu wa kuwajali watotot hao”

Ikumbukwe kuwa maadhimisho ya siku ya Wanawake kwa mkoa wa Katavi yatafanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.