Mpanda FM

Wananchi Katavi waomba elimu zaidi kuhusu gonjwa wa red eyes

10 April 2024, 11:47 pm

Picha na Mtandao

Changamoto inayochangia kuongezeka kwa Ugonjwa huo ni pamoja na baadhi ya Watu kutokufahamu ugonjwa huo unaambukizwa kwa njia ipi

Na Veronika Mabwile -Katavi

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Mpanda  mkoani Katavi  hawana uelewa wa namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa macho mekundu (Red Eyes)

Wakizungumza na Mpanda Redio Fm wakazi hao wamesema kuwa moja ya changamoto inayochangia kuongezeka kwa Ugonjwa huo ni pamoja na baadhi ya watu kutokufahamu Ugonjwa huo unaambukizwa kwa njia ipi

Sauti ya Wananchi wakielezea athari za Ugonjwa huo na kuhitaji elimu zaidi itolewe

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Town clinic DKT Gabriel Rukubigwa amesema kuwa Ugonjwa huo una Madhara Makubwa kwa Binadamu ikiwemo kupofuka Macho

Sauti ya Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Town clinic DKT Gabriel Rukubigwa akielezea ugonjwa huo

Ugonjwa wa Macho Mekundu ni Ugonjwa unaosababishwa na Virusi na dalili zake ni Macho kuwa mekundu ,Kichwa kuuma pamoja na Mgonjwa kushindwa kustahimili Mwaga.