Mpanda FM

Wafugaji wa Nyuki Waomba Ushirikiano kwa TAWA

15 August 2023, 8:31 am

NSIMBO
Uongozi wa wafuga Nyuki katika halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wameiomba serikali Kupitia kamishna wa utunzaji wanyamapori Tanzania TAWA kuwaondolea vikwazo ambavyo vimekuwa Vikiwakwamisha katika shughuli za utafutaji.

Akisoma risala mbele ya kamishna wa TAWA Tazania na Mbunge wa jimbo la NSIMBO mwenyekiti wa uongozi wa wafuga nyuki, ametoa malalamiko hayo Ambapo amesema kumekuwa na msululu wa Kodi, kusafiri umbali mrefu hadi mlele kufuata vibali, na kukatazwa kutumia usafiri wa pikipiki kuingia katika eneo la msitu.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la nsimbo ANNA LUPEMBE amemuomba kamishna wa TAWA kutengeneza mazingira bora ya utendaji kazi baina yao na wananchi, kwani wote wanaishi kwa kutegemeana ili wananchi waweze kupata kipato katika maeneo hayo, na TAWA waweze kuyasimamia maeneo hayo yasivaniwe na kufanyiwa uharibifu.

Akijibu risala hiyo kamishna mkuu wa TAWA Tanzania MABULA M. NYANDA amewahakikishia kuwepo kwa mazingira bora ya ufanyaji kazi baina yao na wanachi Pamoja na kuondoa baadhi ya vikwazo kama kufuata vibali katika wilaya ya mlele, akiagiza kuwepo ofisi eneo la karibu inayoweza kufikika kwa urahisi na wafugaji hao.

Aidha Kamishna huyo ameagiza changamoto zingine kama Kwenda na pikipiki eneo la msitu Pamoja na kupitia upya kodi kifanyike kikao ili kuona uwezekano wa kuruhusu pikipiki Pamoja na kupunguza kodi kabla ya mwezi wa tisa ambapo wafugaji hao wanatarajia Kwenda kufanya uvunaji wa asali