Mpanda FM

Wabeba taka Mpanda wameshindwa kazi?

20 February 2024, 5:24 pm

Picha na Samweli Mbugi

Wananchi wamesema mtaa huo umekuwa na harufu kali ambayo imekuwa haivumiliki na wamekosa namna  ya kufanya hivyo wanahifadhi kwenye mifuko  kwa sababu taarifa za taka hizo wamelalamika kwa viongozi wao bila mafanikio yeyote.

Na Samwel Mbugi-Katavi

Wananchi wa kata ya Majengo mtaa wa Paradise Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wamesema takataka zimekuwa kero kubwa katika mtaa huo na kusababisha funza kuingia ndani ya nyumba zao wanazoishi.

Hayo yamesemwa na wananchi walipokuwa wakizungumzana  Mpanda Radio Fm katika  mtaa huo ambapo wamesema kwa muda mrefu kumekuwa na mrundikano wa taka kwenye mifuko bila kutolewa na mamlaka zinazohusika na uzoaji.

Wananchi wamesema mtaa huo umekuwa na harufu kali ambayo imekuwa haivumiliki na wamekosa namna  ya kufanya hivyo wanahifadhi kwenye mifuko  kwa sababu taarifa za taka hizo wamelalamika kwa viongozi wao bila mafanikio yeyote.

Sauti ya Wananchi wa mtaa wa Paradise wakielezea changamoto ya mrundikano wa taka kwa muda mrefu

Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa huo Magireth Atanasi amekiri kuwepo kwa Mrundikano wa taka kwenye mtaa huo, ambapo amesema viongozi wanaohusika na uzoaji wa taka hizo wamekuwa wakitoa ahadi ambazo hazitekelezeki kwa muda mrefu.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Majengo Magireth Atanasi akielezea changamoto ya taka katika mtaa anaouongoza

Baadhi ya taka zilizorundikana katika mtaa wa Paradise kwa muda mrefu.

Afisa Mazingira wa manispaa Alex Semwali  amesema ni kweli changamoto hiyo ipo lakini wiki hii wanafanya jitihada za kuzoa taka hizo zilizopo kwenye makazi ya wananchi.

Sauti ya Afisa Mazingira wa Manispaa Alex Semwali akijibia changamoto hiyo.

Kadhalika Semwali ameongeza kwa kusema changamoto iliyopelekea mrudikano mkubwa wa taka kwenye makazi ya wanachi ni uhaba wa magari ya kubebea taka hizo.