Mpanda FM
Mpanda FM
2 February 2026, 5:36 pm

“Watu wanaweza kufungua kesi popote pale bila kufika mahakamani”
Na Samwel Mbugi
Mahakama nchini Tanzania imefanikiwa kufanya maboresho ya mifumo ya tehama na kurahisisha upatikanaji huduma za uendeshaji wa kesi kwa njia ya mtandao kama utekelezaji wa dira ya upatikanaji wa haki sawa kwa wote kwa wakati.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Katavi, Gway Sumaye amesema maadhimisho hayo ni kiashiria cha kuanza kazi kwa mwaka kwa kupokea mashauri na kuyatolea maamzi kwa wakati.
Akizungumza mbele ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ambae amemwakilisha mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ameipongeza mahakama kwa kuboresha huduma ikiwemo matumizi ya tehama pamoja na miundombinu ya mahakama hiyo.
Awali akisoma tarifa mbele ya mgeni rasmi mwendesha mashitaka mkoa wa Katavi amesema maadhimisho hayo yanakumbusha dhima na wajibu wa pamoja katika kulinda amani na haki ya kila mwananchi.
Maadhimisho ya mwaka huu kitaifa yamefanyika jijini Dodoma yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayo mchango wa Mahakama katika ustawi na maendeleo ya taifa.