Mpanda FM

Daraja la Msadya lakamilika, laanza kutoa huduma kwa wananchi Katavi

12 December 2023, 10:10 am

Picha na Site Tv

Daraja hilo limegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 4.8

Na Betord Benjamini-Katavi

Daraja la Msadya  lenye urefu wa Mita 60 lilipo katika  halmashauri ya Mlele  mkoani  Katavi limekamilika na limeanza kutoa huduma kwa wananchi.

 Akizungumza Meneja wa TARURA wilaya ya Mlele Mhandisi  Paul Mabaya amesema daraja hilo limegharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.8 na kuahidi kuendelea kutekeleza miradi kwa ufanisi ili pesa zinazotolewa na serikali ziweze kuwanufaisha wananchi.

Sauti ya Meneja wa TARURA Wilaya ya Mlele Mhandisi  Paul Mabaya

 Picha na Site Tv

Awali wakizungumza wananchi pamoja na baadhi ya madiwani wa halmshauri hiyo wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukamilisha ujenzi wa daraja hilo kutokana na usumbufu waliokuwa wanakabiliano nao. .

Sauti ya Madiwani na Wananchi wakipongeza ukamilishwaji wa Daraja hilo