Mpanda FM

Umaskini watajwa chanzo cha ukatili wa kijinsia kwa wanawake Katavi

21 March 2024, 9:32 am

Picha na Mtandao

 “Jamii inapaswa kupewa elimu juu ya namna ya kumwinua mwanamke kiuchumi pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia ili kuwepo na usawa wa kijinsia kati ya mwanaume na mwanamke

Na Rachel Ezekia-Katavi

Umaskini umetajwa kuwa chanzo cha ukatili wa kijinsia kwa wanawake katika jamii na kupelekea ukandamizaji  wa haki kwa kundi hilo mkoani Katavi.

Hayo yameelezwa na wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi  ambapo wamesema uwepo wa mifumo dume na kutowapa fursa za kiuchumi wanawake  kunapelekea kuongezeka kwa matendo ya ukatili dhidi ya wanawake.

Sauti ya wananchi Manispaa ya Mpanda wakieleza mfume dume unavyowaathiri wanawake

Afisa ustawi wa jamii kutoka hospitali ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Malagano Thabiti amesema mifumo dume iliyopo katika jamii inapelekea kuongezeka kwa ukatili wa kijinsia kwa wanawake na kuwataka wanaopitia ukatili kujitokeza ili kupata msaada wa kisheria.

Sauti ya Afisa ustawi wa jamii kutoka hospitali ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Malagano Thabiti

Jamii inapaswa kupewa elimu juu ya namna ya kumwinua mwanamke kiuchumi pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia ili kuwepo na usawa wa kijinsia kati ya mwanaume na mwanamke.