Mpanda FM

KATAVI, TMDA Yabaini Ongezeko la Ugonjwa wa Figo

15 March 2024, 6:01 pm

Kuna changamoto ya Ini na Figo kushindwa kufanya kazi, na Saratani kuongezeka katika Jamii Yanayosababishwa na  matumizi mabaya ya dawa kwa baadhi ya WananchiPicha na Mtandao

Na Samwel Mbugi-katavi

Mamlaka ya dawa na vifaa tiba [TMDA] kutoka makao Makuu Dodoma imetoa Elimu kwa Wananchi wa Misengereni kata ya Ilembo mkoani Katavi kuhusu matumizi sahihi ya dawa na utoaji wa taarifa za maudhi yanayotokana na matumizi ya dawa na vifaa tiba.

James Ndege Afisa mwandamizi wa TMDA amesema kuwa wamefanya utafiti na kubaini kuwa kuna changamoto ya Ini na Figo kushindwa kufanya kazi, na Saratani kuongezeka katika Jamii Yanayosababishwa na  matumizi mabaya ya dawa kwa baadhi ya Wananchi.

Sauti ya James Ndege Afisa mwandamizi wa TMDA

Aidha Ndege  amesema kuwa baadhi ya watu wanachanganya kwa wakati mmoja tiba ya Hospital na tiba Asili jambo linalopelekea kuchosha Figo na Ini ambapo baadhi ya wananchi huamini kuwa dawa za asilia hazina kemikali.

Sauti ya James Ndege Afisa mwandamizi wa TMDA

Kwa upande wa Wananchi wameshukuru kutolewa kwa Elimu hiyo ambapo awali walikua wanatumia dawa bila kufuata taratibu za kitabibu na Elimu hiyo imekuwa mkombozi.

Sauti ya wananchi wakieleza kuhusu elimu waliyoipata ya matumizi ya dawa.

Katika hatua nyingineJames Ndege ametoa wito kwa Wananchi wanaoenda kupata matibabu Hospital kuhakikisha matibabu wanayapata wanakamilisha dozi  bila kuchanganya na tiba nyingine.