Mpanda FM

Ulinzi, usalama waendelea kuimarishwa Katavi

11 April 2024, 12:36 am

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko. Picha na Anna Milanzi

Baraza kuu  la Waislamu    wanaupongeza uongozi wa   Mkuu wa  Mkoa kwa kuhakikisha hali ya utulivu inaimarika

Na Lilian Vicent-Katavi

Wananchi wa mkoa wa Katavi Wamehakikishiwa usalama wakati wa kufanya shughuli za kijamii na kiuchumi kwa kuwa jeshi la polisi lipo imara katika kuimarisha ulinzi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Mwanamvua  Hoza Mrindoko ambaye pia ni Mgeni Rasmi katika hafla ya Iftari ilyoandaliwa na Jeshi la Polisi April 9 iliyofanyika  katika Ukumbi  wa  Polisi  Club  Mkoani Katavi  

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza

Kwa Upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa  wa Katavi Mashaka Nassoro Kakulukulu amesema kuwa wao kama Baraza kuu  la Waislamu    wanaupongeza Uongozi wa   Mkuu wa  Mkoa kwa kuhakikisha hali ya Utulivu inaimarika.

Sauti ya Sheikh Mkuu wa Mkoa  wa Katavi Mashaka Nassoro Kakulukulu akiipongeza kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa

Nae kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa  ameshukuru  Ushirikiano unaotolewa na Wananchi katika kukomesha Matukio ya  Kihalifu  na kuwataka kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoani hapa ili kutokomeza Matukio ya Kihalifu.

Sauti ya Kamanda wa Jeshi la Polishi Mkoa wa Katavi