Mpanda FM

Martha Afurahishwa Kukamilika kwa Kituo cha Afya Ugalla

26 July 2023, 5:43 pm

NSIMBO.

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki ameishukuru serikali Kwa kutoa fedha Shilingi Milioni 590 Kwaajili ya kufanikisha ujenzi wa Kituo Cha afya Ugalla Halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi.

Akizungumza na Wananchi katika Kijiji Kasisi Kata ya Ugalla wakati wa ziara ya kutembelea Kata za Mkoa wa Katavi Amesema kuwa Kitendo Cha serikali kujenga Kituo Cha Afya Ugalla utakwenda kuwakomboa wananchi kupata huduma karibu na adha ya kupata Huduma za Afya katika Kituo Cha Afya Kanoge ambacho kipo mbali kutoka Kijiji Cha Ugalla.

Ameeleza kuwa Maendeleo yanayoonekana katika Kata hiyo na Jimbo la Nsimbo Kwa ujumla inatokana na kuchagua Viongozi wenye Uchu wa kuwaletea wananchi Maendeleo wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna lupembe.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ugalla ambae ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Charles Halawa amesema kilio Cha Wana ugalla kilikuwa ni Kupata Kituo Cha Afya ambacho tayari serikali imejenga.

#mpandaradiofm97.0

#ccm

#wizarayaafya