Mpanda FM

Wazee Uwanja wa Ndege Waonya Vikundi Vya Uhalifu

19/11/2021, 12:23 PM

Wazee wa kata ya uwanja wa Ndege  Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamewashauri wazazi na walezi katika kata hiyo  kuwaeleza watoto juu ya madhara  yatokanayo  na kujihusisha na makundi ya kiuharifu

Wakizungumza na kituo hiki  mara baada ya kikao na diwani wa kata hiyo Maiko Kamande Mbogo wazee hao wamesema ili kata hiyo isiwe na makundi ya watoto wenye tabia za udokozi na vitendo vingine vya uharifu ni lazima wazazi  kuwajibika ipasavyo

Sauti za Wazee

Kwaupande  wake diwani  Maiko Kamande Mbogo akizungumza juu ya baadhi ya watoto kushiriki katika makundi ya kiuharifu amesema kuwa inatokana na baadhi ya wazazi na walezi kujisahau wajibu wao.

Sauti ya Diwani

Kata ya uwanja wa ndege inajumla ya mitaa mitatu ambayo ni  Mtaa wa msufini ,mtaa wa Airtel na mtaa wa mnazi mmoja.