Mpanda FM
Mpanda FM
1 January 2025, 9:04 pm

“kupitia sera ya utawala bora wamejipanga kutambua makundi ya watu wenye ulemavu kwani wamekuwa wakisahaulika katika jamii“
Na Samwel Mbugi – Katavi
Baadhi ya watu wenye ulemavu Kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameshiriki chakula cha pamoja kilichoandaliwa na diwani wa kata hiyo Hamisi Misigalo kwa kushirikiana na wenyeviti wa mtaa wa Msasani ,Tambukareli na Mpanda hotel .
Wakizungumza katika hafla hiyo wametoa shukrani kwa diwani kuwa na moyo ya kuwakumbuka watu wenye ulemavu katika siku ya mwaka mpya kwa kuandaa chakula cha pamoja.
Sauti ya watu wenyeulemavu
Hata hivyo kwa upande wake Godfrey Albeto Sadala katibu wa chama cha wenye ulemavu mkoa wa katavi ametoa shukrani kwa diwani kwa kuandaa chakula cha pamoja na kundi hilo na kubaini changamoto zao zinazowakabili.
Godfrey Albeto Sadala katibu wa chama cha walemavu mkoa wa katavi
Kwa upande wake Ibrahimu Mzanda mwenyekiti wa mtaa Mpanda Hotel akiwawakilisha wenyeviti wa mitaa ya Msasani na Tambukareli amesema kuwa kupitia sera ya utawala bora wamejipanga kutambua makundi ya watu wenye ulemavu kwani wamekuwa wakisahaulika katika jamii.
Sauti ya Ibrahimu Mzanda mwenyekiti wa Mpanda Hoteli
Hamisi Misigalo diwani wa kata ya Mpanda Hotel amesema baada ya kutambua kuwa uongozi uliopita haujawahi kukaa na kundi hilo na kuandaa chakula cha pamoja akaona ni vyema kufanya hivyo ili na wao waone wanathaminiwa katika jamii.
Sauti ya Hamisi Misigalo diwani wa kata ya Mpanda Hoteli

Diwani misigalo ameahidi kutoa viti mwendo vinne kwa wenye ulemavu wa Kata hiyo, kushughulikia bima, masuala ya TASAF pamoja na mikopo ya asilimia kumi kwa wenye ulemavu.