Mpanda FM
Mpanda FM
28 April 2026, 12:35 pm

“Usiogope maisha na usiyakimbie majukumu”
Na Restuta Nyondo
Wazazi wametakiwa kujiandaa na kupanga uzazi kabla ya kufanya maamuzi ya kupata watoto ili kuepukana na changamoto ya baadhi ya wanawake kutupa watoto wao baada ya kujifungua.
Hayo yamesemwa na afisa taarafa ya Misunkumilo Leah Gawaza wakati walipo tembelea na kutoa msaada katika kituo cha watoto yatima cha Mtakatifu Yohane wa pili kilichopo kata ya Nsemulwa Wilayani Mpanda Mkoani Katavi Kupitia kampeni ya TUWAGUSE ambapo kupitia kampeni hiyo wamefanikiwa kukusanya fedha na mahitaji yenye thamani ya shilingi 4,580,000 .
Baadhi ya wanawake walioshiriki katika kampeni hiyo wamesema kuwa jukumu la kulea watoto ni la jamii nzima na kutoa wito kwa makundi mbalimbali kuendelea kujitolea katika kuwasaidia watoto hao.

Mkuu wa kituo cha watoto yatima cha Mtakatifu Yohane wa pili Sister Rose Sungura amewashukuru wote walioguswa na kushiriki kampeni hiyo na kuendelea kuomba jamii kushiriki katika malezi ya watoto katika kituo hicho.
Kampeni ya TUWAGUSE iliyoanzishwa na Leah Gawaza inalenga kuhamasisha jamii kushiriki katika kusaidiana kutatua changamoto za kiutu,ushauri na kukuza kipato kwa wasiojiweza.