Mpanda FM

Wananchi Mkoani Katavi wachukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa Wa Kipindupindu

18 January 2024, 12:00 am

Picha na Mtandao

Tahadhari    wanazotakiwa kuchukua Wananchi ili kujiepusha  na Ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kutumia Vyoo bora.

Na Lilian Vicent-Katavi

Baadhi ya Wananchi  wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni  mseto juu ya tahadhari wanazozichukua kuhakikisha wanajikinga na Ugonjwa wa Kipindupindu.

  Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti  wakati wakizungumza na Mpanda Redio Fm  na kubainisha kuwa    wanasafisha mazingira yanayowazunguka na kuhakikisha Chakula wanachokitumia ni safi na salama.

Sauti za Wananchi wakieleza uelewa wao na tahadhari wanayochukua dhidi ya Ugonjwa wa kipindupindu

kwa upande wake Afisa afya Manispaa ya  Mpanda   Eric Kisaka amebainisha kisababishi cha ugonjwa wa Kipindupindu na tahadhari    wanazotakiwa kuchukua Wananchi ili kujiepusha  na Ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kutumia Vyoo bora.

 Sauti ya Afisa afya akibainisha sababu za Ugonjwa wa Kipindupindu

Afisa afya Kisaka amewashauri Wananchi kuhakikisha mazingira yanakuwa safi  ili kuepuka kusambaa kwa vimelea vya Ugonjwa huo wa Kipindupindu.

Sauti ya Afisa afya akisisitiza Wananchi kufanya usafi