Mpanda FM

Akutwa amefariki kwenye bajaji Mpanda

8 November 2023, 1:19 pm

Picha na Mtandao

Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 50 amekutwa amefariki dunia katika eneo la Rugwa.

Na Gladness Richard – Mpanda

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina Hillalie Rioba mwenye umri wa miaka 50 amefariki dunia katika eneo la Rugwa kata ya Kazima manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Akizungumza na Mpanda Radio fm mke wa marehemu amesema kuwa alipokea taarifa ya kifo cha mume wake asubuhi kutoka kwa majirani zake.

Sauti ya Mke wa Marehemu

Hata hivyo  mwenyekiti wa mtaa wa Rugwa George Mwelela amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kwenye eneo lake na amesema kuwa marehemu alikuwa anajishughulisha na kazi ya ulinzi.

Sauti ya Mwenyekiti

Mpanda radio fm bado inaendelea kufanya jitihada ili kuzungumza na kamanda wa jeshi la polisi  Mkoani hapa kubaini chanzo cha kifo hicho.