Mpanda FM

Wananchi Karema wafikisha kilio chao kwa RC Katavi

29 March 2024, 2:30 pm

Wananchi wa kata ya Karema wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi wakiwa katika Mkutano .Picha na Anna Milanzi

Upepo mkali uliovuma Machi 16 na March 24,  2024 na maji  ya ziwa Tanganyika kuingia katika makazi ya watu , jumla ya kaya 220 zimekumbwa na changamoto hiyo ambapo nyumba 62 zimebomoka na wahanga wamehifadhiwa kwa ndugu na majirani huku familia tano zikijihifadhi katika shule ya msingi shikizi Mwenza 

Na Anna Milanzi -Katavi

Wananchi wa Kata ya Karema Wilayani Tanganyika mkoani Katavi wameomba msaada zaidi kutokana na nyumba zao kuzingirwa na Maji yanayotoka katika ziwa Tanganyika huku sababu hasa ikiwa ni mabadiliko ya tabianchi.

Wameyasema hayo walipotembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi  katika kata hiyo huku akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama na viongozi wengine wa Mkoa ambapo wameishukuru serikali kwa misaada ya Chakula, Mboga ,Chandarua,pamoja na dawa za kutibu Maji

Sauti ya Wananchi Kata ya Karema wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutamatika kwa mkutano huo

Diwani wa Kata ya Karema  Marko Kapata ameiomba  serikali kulindwa kwa Kijiji hicho kwa kuwawekea Mifereji na tuta la mawe ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Karema  Marko Kapata akitoa ombi la kuwekewa Mifereji na tuta la Mawe ili kuthibiti changamoto hiyo

Diwani ya Kata ya Karema .Picha na Anna Milanzi

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ametoa pole kwa Wananchi na kueleza kuwa uchunguzi utafanyika ili kuweza kubaini sababu za kutokea kwa changamoto hiyo ili waweze kuchukua hatua stahiki.

Sauti Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza na Wananchi wa kata ya Karema

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza na Wananchi kata ya Karema.Picha na Anna Milanzi

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mtendaji wa kata hiyo David Kwilasa imeeleza kuwa upepo mkali uliovuma March 16 na March 24,  2024 na maji  ya ziwa Tanganyika kuingia katika makazi ya watu , jumla ya kaya 220 zimekumbwa na changamoto hiyo ambapo nyumba 62 zimebomoka na wahanga wamehifadhiwa kwa ndugu na majirani huku familia tano zikijihifadhi katika shule ya msingi shikizi mwenza  na kueleza changamoto kama hiyo ya maji  ya ziwa Tanganyika kuingia  katika makazi ya watu imewahi kujitokeza kwa Mwaka  2021. Kuona taarifa hii kwa youtube channel yetu bonyeza hapa