Mpanda FM

Wananchi waaswa juu ya usafi wa mazingira

15 December 2023, 2:23 pm

Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko akiongoza zoezi la usafi. Picha na Maktaba

Wananchi Katavi washauriwa kuweka mazingira katika hali ya usafi ili kutokomeza mazalia ya mbu.

Na Leah Kamala – Mpanda

Wananchi Maanispaa ya Mpanda mkoani Katavi  Katavi wameshauriwa kuweka mazingira katika hali ya usafi ili kutokomeza mazalia ya mbu katika msimu huu wa mvua.

 Wakizungumza na Mpanda radio fm wamesema kuwa kutokana na msimu wa mvua unaoendelea  wamekuwa wakichukua tahadhari ikiwemo kusafisha mazingira kwa kufukia madimbwi, kufyeka nyasi ndefu pia kutumia vyandarua vyenye dawa ili kujikinga Na ugonjwa wa malaria.

Sauti ya Wananchi

Aidha Kwa upande wa afisa afya Manispaa ya Mpanda ERICK KISAKA Amesema kwa upande wa serikali wamekuwa wakitoa elimu kwa jamiii  namna ya kutunza mazingira ili kutokomeza mazalia ya mbu na kuitaka jamii kuendelea kuifadhi mazingira ikiwa ni hatua ya kujikinga na ugonjwa wa malaria.

Sauti Erick Kisaka